Proverbs 6:1-5

Maonyo Dhidi Ya Upumbavu


1 aMwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,
ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi
kwa ajili ya mwingine,

2 kama umetegwa na ulichosema,
umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

3 basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,
kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:
Nenda ukajinyenyekeshe kwake;
msihi jirani yako!

4 bUsiruhusu usingizi machoni pako,
usiruhusu kope zako zisinzie.

5 cJiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji,
kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.

Copyright information for SwhKC